| ||||
Baada ya Wajerumani kuangushwa duniani pote katika Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia (1914 – 1918), Tanganyika, iliyokuwa sehemu ya Dutch East Africa (nchi nyingine katika eneo hili zikiwa Rwanda na Burundi) iliwekwa chini ya utawala wa Waingereza kama wadhamini. Nchi haikuwa koloni kama ilivyokuwa Kenya, Nyasaland( Malawi) na Northern Rhodesia (Zambia). Kwa maeneo ya kusini hali ilikuwa kama Wadachi waliwaambia cha kuwafanyia wenyeji wa kusini. Hakuna kumbukumbu zinazoonyesha kwamba watawala wapya walikuwa na mipango au azma ya kuendeleza eneo hilo katika fani mbali mbali. Yaliyotokea yalilenga kunufaisha watawala. Baada ya vita Waingereza walikuwa wachovu kiuchumi hali ya huduma za kijamii ziliathirika na vita. Kampuni iliyoitwa Overseas Food Corporation ilianzisha mradi mkubwa wa kulima karanga Urambo (Tabora) Kongwa (Dodoma) na Nachingwea (Lindi). Ili kuhudumia mashamba kwa ufanisi bandari ya Mtwara iliboreshwa. Wakati huo huo wakajenga reli na bomba la mafuta toka bandarini Mtwara hadi Nachingwea. Reli ilikuwa ienddelee hadi Mbamba bay pwani ya ziwa Nyasa. Mnamo mwezi Oktoba 1961 lilifunguliwa tawi la reli la kilomita takribani 40, toka Chilungula hadi Masasi. Miundombinu na shughuli za kilimo zilitoa ajira na maeneo yaliyopitiwa na miundo msingi hiyo yalifunguka kwa maendeleo Kwa sababu mbali mbali mradi wa karanga Nachingwea ulifungwa. Mwaka mmoja baada ya Tanganyika kupata Uhuru, sarikali ya Tanganyika huru ikaamini kuwa reli na bomba la mafuta vilikuwa ni miradi isiyo na tija. (white elephant). Reli na bomba vikang’olewa. Athari za hatua hiyo ni bayana .Kusini kulizidi kuzama kimaendeleo, taswira iliyodumu kwa kipindi kirefu. Lakini kwa muda mfupi watawala (Waingereza) walimaizi kwamba eneo la kusini lilikuwa na utajiri mwingi hivyo wakaita “Cinderella Province” Cinderella ikiwa na maana ya ‘mtu au kitu ambacho uzuri au uwezo wake haujatambulikana”. Jingine walilolifanya Waingereza ni kuangusha magogo na kupasua mbao huko Rondo Mnara (Lindi vijijini). Kampuni iliyoitwa Steel Brothers ilifanya kazi hiyo miaka ya 1950. Wakavuna , wakachuma na kuondoka . Wananchi wakaachiwa visiki vya mipingo , mbambakofi,mivule nk. wakati huo huo walikumbatia umasikini. Kusini baada ya uhuru. Miaka michache ya kuelekea uhuru kulianzishwa mradi mkubwa wa maji toka mto Ruvuma ,uliendeshwa na kampuni ya Makonde Water Corporation. Ilipangwa maji yaenezwe sehemu mbalimbali huko kusini. Miaka michache baada ya kuasisiwa kwa vishindo mradi ulikufa. Wananchi hawakuelezwa sababu za mabadiliko hayo. Madhila,taabu na kero za kukosa maji hazikumilithika . Katikati ya miaka 1960 kulizuka mgogoro wa kiwanja katika mji mdogo wa Mahuta (wakati huo Newala , sasa uko katika wilaya ya Tandahimba ). Mfanyabiashara wa Kiasia alipora eneo hilo ili ajenge kituo cha mafuta ya nishati. Wananchi wakachachamaa. Uongozi wa mkoa na wilaya ukaingilia kati. Kwenye mkutano wa hadhara hapo Mahuta , kiongozi wa wananchi alipigwa viboko kwa sababu za “kupinga hatua za maendeleo “ kama walivyoita watawala. Kupinga uonevu kunyanyaswa na kudharauliwa, wananchi waliandika barua ngazi za juu za taifa na kudai , moja , mkuu wa mkoa na yule wa wilaya wahamishwe ,mbili, wapendekeze majina ambayo yatatoa mkuu wa mkoa na yule wa wilaya ; na tatu kama maombi hayo hayatakubalika watajitenga na kujiunga na Msumbiji ili wawe pamoja na FRELIMO kutafuta ukombozi. Yaliyofuata ni historia. Miaka mitatu baada ya uhuru wa Tanganyika , wana Msumbiji kupitia FRELIMO walianzisha vita vya ukombozi. Kutokana na mazingira ya kijiografia ( kati ya nchi mbili ) eneo lote la kusini likawa “no go area” – hapakuwa na shughuli zozote za maana za kimaendeleo zilizokuwa zikifanyika . FRELIMO wakafanikiwa kukunja jamvi ukoloni mwaka 1975. Ni dhahiri kwa miaka kumi wengine walikuwa wamesonga mbele hapa nchini . Mategemeo na matumaini ya wengi huko kusini ni kuwa serikali ingekuwa na programu maalum “kufidia muda uliopotea”. Wakati wa Vita kuu ya Pili vya dunia Yugoslavia ilipambana na majeshi ya Adolf Hitler . Marshal Josef Tito akawaambia wapiganaji wale “ The wounded should not be left behind “ ( majeruhi wasiachwe nyuma). Kimaendeleo kusini ilijeruhiwa na kuachwa nyuma. Barabara ya Dar es salaam – Lindi ni “mkunga” wa matatizo ya kusini. Ahadi za serikali kuijenga zimechukua kipindi kirefu kutekelezwa. Miaka ya 1970 – 80 kampuni moja ya Kitanzania na taasisi moja ya serikali waliteuliwa kujenga barabara hiyo. Wakajenga makambi Nangurukuru (Kilwa).Hakuna ushahidi wa kazi iliyofanywa – tatizo la barabara likawa “ kichwa cha mwenda wazimu”. Mwaka 1977 wananchi wa kusini, wakiungwa mkono na wa maeneo mengine, waliasisi mchango maalum kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo. Mwitikio wa wito huo ulikuwa chanya. Ofisini ya Waziri Mkuu ikasitisha zoezi hilo kwa ahadi kuwa serikali igejenga mradi huo. Imechukua miongo kadhaa kukamilika kazi hiyo. Miaka ya 1960 – 70 wananchi wa kusini walihamasishwa kulima korosho kwa ajili ya biashara. Matokeo yalikuwa ya kutia moyo. Mapori yalipisha mashamba ya mikorosho. Zao likachangia umasikini. – Pembejeo bei juu na soko likawa halina uhakika . Kuna viwanda vya kubangua korosho Masasi , Newala Lindi na Mtwara lakini hakuna msimamo maalum wa Bodi ya Korosho na wanasiasa wa kuuza nje zao lililoongezewa thamani. Bado wanakumbatia fikra hafidhina zilizopitwa na wakati wa kuuza nje ya nchi korosho ambazo hazijabanguliwa. | ||||
MASASI NDIO HOME
Sunday, February 24, 2013
HISTORIA YA MTWARA
MAGONJWA HAYA CHANZO CHA MIKOROSHO KUDUMAA

KOROSHO
ni zao muhimu la biashara katika nchi yetu kwani linampatia mkulima
kipato na kuliingiza taifa fedha za kigeni zinazotokana na mauzo ya zao
hilo ndani na nje ya nchi. Kwa
kawaida miti ya mikorosho inastawi vizuri katika ukanda wa Pwani ya
Bahari ya Hindi. Zao hilo hapa Tanzania linalimwa na wakulima wadogo
ambao wana miti mikorosho kati ya 60 mpaka 80.
Mikoa inayolima korosho ni Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga na Ruvuma katika wilaya ya Tunduru. Mikoa mingine ambayo imeanza kulima korosho kwa kiwango kidogo katika maeneo yenye hali ya hewa inayofaa kwa kilimo cha zao hilo ni mkoa wa Mbeya, Njombe, Iringa, Morogoro, Dodoma, na Singida.
Mikoa inayolima korosho ni Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga na Ruvuma katika wilaya ya Tunduru. Mikoa mingine ambayo imeanza kulima korosho kwa kiwango kidogo katika maeneo yenye hali ya hewa inayofaa kwa kilimo cha zao hilo ni mkoa wa Mbeya, Njombe, Iringa, Morogoro, Dodoma, na Singida.
Uzalishaji
wa juu wa korosho katika msimu wa mavuno wa mwaka 1973/74 ulifikia tani
145,000 za korosho ambazo kwa sehemu kubwa zilisafirishwa kwenda India.
Magonjwa ni kikwazo
Mbali
na hayo zipo changamoto mbalimbali ambazo zinasababisha baadhi ya
wakulima kukata tamaa kwa mfano kuwapo kwa ugonjwa unaoshambulia zao
hilo.Mkoani Mtwara, kuna kituo
cha utafiti wa magonjwa yanayoshambulia zao hilo cha Naliendele ambacho
kinafanya utafiti ili kubaini magonjwa na wadudu waharibifu, na kutafuta
ufumbuzi.
Dk
Louis Kasuga ni mtafiti wa kituo hicho anasema ugonjwa wa Ubwiri,
ulionekana ni tatizo kubwa katika kilimo cha korosho. Katika Miaka ya
karibuni pia ugonjwa wa blaiti nao umeonekana kushambulia zaidi zao hilo
na kwamba hivi sasa magonjwa hayo yamepatiwa dawa za kudhibiti magonjwa
hayo.
Dk
Kasuga anasema tatizo lingine ni gugu tegemezi (dodder) ambalo limekuwa
likiota kwenye maeneo ya Mtwara, Lindi, Kilwa, Rufiji, Mkuranga,
Bagamoyo, Pangani, Tanga na Mkinga. Gugu hilo ni chanzo chake ni mbegu
iliyoota na kutegemea mmea mwingine kama miti ya mikorosho kustawi.
Utafiti
uliofanywa na Kituo cha Naliendele kwa kikishirikiana na Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam umethibitisha kuwa gugu hilo linastawi vizuri katika
ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi. Dk
Kasuga anasema mbali ya gugu hilo kushambulia mikorosho pia
linashambulia mazao mengine kama michungwa, miti ya membe, mimea
mingine.
Wakulima
wanatambua kuwapo kwa tatizo hilo, lakini uelewa kuhusu chanzo cha
tatizo hilo numekuwa ni utata na namna ya kudhibiti bado limekuwa ni
kitendawili.
“Gugu
hilo halina majani hivyo halina uwezo wa kujitengenezea chakula chake
chenyewe, kwa msingi huo huishi kwa kutegemea mimea mingine ili liweze
kupata chakula ikiwa ni pamoja na miti ya mikorosho,” anasema mtaalamu
huyo.
Gugu lapunguza uzalishaji
Anasema gugu hilo linadumaza na
kunyonya chakula cha mimea mingine na kwamba gugu hilo linaweza
kusababisha mmea kufa au kukauka. Dk Kasuga anasema gugu hilo linasambaa kwa urahisi zaidi kwa njia ya upepo, maji, ndege, na wanyama.
Anasema gugu hilo linapunguza uzalishaji wa korosho kwa asilimia 100 kwa sababu linategemea miti ya mikorosho kupata chakula.
“Hii
ni kwa sababu ya ushindani wa chakula, maji na jua naa gugu hilo
linakuwa na lina nguvu kubwa ya kunyonya maji na chakula kutoka katika
mti wa mkorosho, hali hiyo inapunguza kipato cha mkulima kutokana na
kushuka kwa mavuno ya korosho,” anasema. Anasema gugu hilo linasababisha umaskini wa kipato na chakula katika kaya na kupunguza kipato cha fedha za kigeni kwa taifa.
Anabainisha
kwamba mbegu za gugu tegemezi zinauwezo wa kukaa chini ya ardhi kwa
miaka kumi bila kupoteza uwezo wa kuota na hivyo linaonekana kuwa sugu. Kwa
mujibu wa tovuti mbali mbali, mbegu za gugu tegemezi ni ngumu kufa
kwani hata wanyama wakila na kutoa kinyesi zinauwezo wa kuota.
Dk Kasuga
anasema njia za kudhibni gugu hilo ni kutoa kambakamba zake kwa
kuzivuta, ingawa gugu hilo limekuwa likirejea kwenye mti uliopo karibu
na gugu. Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Pwani, Robinso Wanjara anasema uongozi
wa Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na kituo cha utafiti cha magonjwa ya
korosho kimewapa maelekezo maofisa kilimo ngazi za kata ili wakachungeze
ukubwa tatizo hilo.
“Tunaamini
kuwa wataalamu wetu tuliowatuma kwenda kwa wakulima watatuletea takwimu
sahihi na kuzipeleka kwenye kituo cha Naliendele kwa ajili ya utafiti
zaidi,” anasema Wanjara.
Anasema
kutokana na kuwapo kwa gugu hilo katika Mkoa wa Pwani, anasema kuwa
kiwango cha uzalishaji kimekuwa kikisuasua na kusabaisha wakulima kupata
mavuno kidogo.
“Katika
mkoa wetu huu wa Pwani zao tunalolitegemea kwa ajili ya biashara ni
korosho likifuatiwa na muhogo, matunda, na mbogamboga sasa
linavyoathiriwa na gugu hilo linasababisha Mkoa wa Pwani uathirike
kimapato,”amesema.
Wakulima wazungumzia gugu tegemezi
Niliweza kupata fursa ya kuzungumza na
baadhi ya wakulima wa zao la korosho kutoka katika Kijiji cha Malendego
kilichoko Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi juu ya namna wanavyolitambua
hili gugutegemezi na njia wanazozitumia katika kukabiliana nalo Mkulima
wa Kijiji cha Malendego wilayani Kilwa, mkoani Lindi, Omary Mtunyungu
anasema gugutegemezi limemuathiri kiuchumi na kwamba umasikini unabisha
hodi katika familia yake.
Mtunyungu anasema kutokana na hali
hiyo ametoa taarifa kwa wataalamu wa kilimo ili kupata msaada wa
ufumbuzi, lakini mpaka sasa tatizo halijatatuliwa.
“Inaonekana
idadi ya wataalamu wa kilimo ni ndogo kwa sababu sisi wa huku kijijini
hatufikiwi na huduma hiyo naomba serikali ijitahidi kuongeza idadi ya
wataalamu ili watusaidie jinsi ya kukabiliana na vikwazo vya kilimo hasa
magonjwa .
Mkulima
na mkazi wa Kijiji hicho cha Malendego, Mohamedi Mtauka anasema amekata
tamaa kuongeza kilimo cha zao hilo kwa kuwa gugutegezi limeathiri sana
mimea yake ya korosho na kusababisha kipato chake kushuka.
Asili
ya kilimo cha zao la korosho ni kutoka nchi ya Brazil iliyopo Amerika
ya Kusini na liliingizwa Tanzania katika karne ya 16 kutokea Msumbiji
ambako lilikuwa likilimwa na Wareno.
Subscribe to:
Comments (Atom)