Sunday, February 24, 2013

MASASI WATUPILIA MBALI UTAMADUNI


Ninakililia kizazi hiki cha watumwa wa fikra, wanaofikiria mila na desturi za jadi kuwa zimepitwa na wakati, wenyewe wanajiita KIZAZI CHA DOTCOM, kizazi kisichokuwa na utamaduni kisichojua wanakotoka wala wanako kwenda mithili ya mtu aliyefungwa kitambaakizito usoni.

Wanamasasi hivi kwanini wanashindwa kuendeleza utamaduni wao mzuri na wenye kuvutia kama vile jando na unyago, ngoma za asili na hata michezo ya jadi kama CHAKO, KOMBOLELA, KAMPIYOPIYO NA BOLITILITI.

Mtakubaliana nami kuwa wilaya ya masasi katika miaka ya michache iliyopita ilikuwa kinara wa kufufua utamaduni wake, hasa ngoma za asili iliwemo marimba, liwayawaya, sogea, mkala, mwahierani, singenge na ngoma kadha wa kadha ambazo ziliipatia umaarufu wilaya yetu ya masasi hasa panapokuwepo na maonesho au maadhimisho ya kitaifa.

Vijana kutoka vijiji mbalimbali vya wilayani Masasi walionesha juhudi kubwaa katika kuanzisha vikundi vya ngoma za asili vilivyo weza kukonga nyoyo za watu wengi, mfano mzuri ni vikundi cha ngoma ya liwayawaya kutoka katika vijiji vya Tukaewote, Temeke, Marokopaleni na Mchoti.

 Pia kikundi cha ngoma ya mwaiherani kutoka Mchauru Mwitika kiliweza kuteka hisia za watu wengi kutokana na uwezo wao wa kuvamia jukwaa mithiri ya siafu wenyenjaa na kuimba tenzi nzuri zenye kufurahisha na kuelimisha jamii.

Vijana wa masasi mjini nao hawauwa nyuma walijitahidi wakaanzisha kikundi cha utamaduni kilicho julikana kama MCHEMA CULTURAL GROUP.Sina uhakika kama kikundi hiki kilichojibebea umaarufu kwa muda mfupi kama kipo hai ama kimekufa.

Vikundi hivyo vya sanaa viliweza kutumbuiza katika shughuli mbalimbali za kiserikali na sherehe za kitamaduni kama vile harusi na unyago na tafrija za kidini kama ubatizo, komuniyo na kipaimara.


Nimeamini msemo usemao "UKISTAAJABU YA MUSA UTAYAONA YA FIRAUNI", siku hizi Masasi hakuna mafunzo ya jadi kwa watoto (JANDO) kwa kile wanachodai kuwa ni kwenda na wakati, siku hizi vijana wakishapata sunnah (TOHARA) hawapelekwi katika chuo kikuu cha jadi (jando) kuandaliwa kushika majukumu ya watu wazima.

Mwisho ninatoa wito kwa wanamasasi kuangalia ni namna gani wanavyoweza kufufua utamadunu wao, maana hali siyo mzuri, vijana wa sikuhizi hawajui DOMIDOMI, MANYASI ULUMU, VIRAVIRA, SUKUTUMPWEMBWE WALA NATURA; INASIKITISHA

No comments:

Post a Comment