Sunday, February 24, 2013

HISTORIA YA MASASI IMEPOTEA


NA COSMAS JARIBU

         Ukifikawilayani Masasi na ukakosa udadisi hutaweza kutambua kuwa eneohilo linavivutio vingi vya utalii ambavyo vimelalausingizi na kuwa mji huo unamuungano mkubwana biashara ya utumwa iliyoungana na uanzishwaji wa Kanisa la Anglikana na hata hospitali ya wilaya (MKOMAINDO).

Wadau wa masuala ya kijiografia, utalii na historia wilayani humo wanaamini kuwa kama kungekuwapo juhudi katikasekta ya utalii ungekuwa moja ya chanzo cha mapato, japodogo kwa halmashauri na kwa wananchi vilevile kama wakishirikishwa. Achiliambali kujenga fursa za kielimu kwa watoto ambao hawaijui vizuri historia ya wilaya yao na nchi kwa ujumla.

Kwamfano, vijana wengi wanaoishi mjini Massi hawajui historia ya hospitali ya Mkomaindo na uhusiano wake na biashara ya utumwa na uanzishwaji wa dhehebu la Anglikan katika eneo hilo na hatimaye kuanzishwa kwa kanisa kuu –Cathedral mjini Masasi.
Wengine hawajui kwanini eneo jingine jirani na hospitali hiyo, katika barabara iendayo Nanyumbu panaitwa Rest Camp na kuwa kwanini kuna kitongoji Mjini Masasi kinachoitwa Nyasa (eneo ambalo wahamiaji waliokuwa watumwa kutoka Malawi/Nyasa walianzisha makazi yao hivyo eneo hilo likabaki na jina hilo hadi leo.)

Wengine hawajui historia ya magofu ya safu za nyumba za wafanyakazi zilizopo katika kitongoji cha nyasa maarufu kama mabatini. Magofu haya yalikuwa ni makazi ya wafanyakazi wa serikali ya wakoloni wa kiingereza, yaliyojengwa mnamo mwaka 1925 baada ya kuanzishwa rasmi Halmashauri ya wilaya ya masasi.
  
Kutokana na kutokuwa na makumbusho ya kihistoria kumbukumbu ya Masasi imebaki kwenye vichwa vya watu ambao kwa umri wamezeeka na huenda wakatoweka kabla ya kuiacha kumbukumbu hiyo adhimu katika maandishi, picha au video.

Masasihaina jumba la makumbusho na ukitaka kujua historia ni lazima uwatembelee wazee kutoka kijiji kimoja hadikingine . Kuna maeneo mazuri ya utalii wakimazingira kwamfano, milima ya miamba ya mawe magumu ambako watu wangeweza kufanyia sherehe au kwenda kuzulu.

Nilipata bahati ya kupelekwa msituni, kiasi cha kilomita tano kutoka mjini kuangalia kaburi la mwaka 1891, la Rev. Father Theophilus Lupton Taylor aliyesimamia kanisa ambalo limezaa Kanisa Kuu la Masasi- Cathedral, cha kushangaza hakuna anayepatunza mahali hapo penye historia hadhimu.

Kuna Waafrika wengi waumuni wa awali wakanisa, lakini hawajulikani ni kina nani kwa hiyo historia ya kipekee yamahali hapo inapotea.

Kama Masasi palikuwa moja ya kituo cha wasafirishaji watumwa na kuwa kanisa lilianza mahali ambako watumwa walikuwa wakitupwa kwa kudhoofu na maradhi na kuwa hospitali ya wilaya kilianza kama kituo cha kujitolea cha kutibu watumwa hao na ni ukweli kuwa karibu na hospitali yawila ya, Mkomaindo kuna makaburi ya watu waliozikwa mwaka 1891- kwa mfano, bwana mmoja aliyekuwa akiitwa Sayed Austin, kwanini basi tusiwe najuhudi za makusudi za kuanzisha kituo japo kimoja kimoja cha kihistoria cha kuwawezesha wageni kufika na kuyajua hayo yote kwa wakati mmoja?

Nyuma ya mlima kwenye kaburi la mmoja wa machifu wa eneo hilo, MwenyeNamkumba. Inaonekana bado anakumbukwa lakini ni lichoona ni mahala tu ambako kumelimwa na kusilibwa kwa udongo wamfinyazi. Lakini hakuna alama ya kaburi lilipo wala utambulisho. Pamezungukwa na kichaka cha kuweza kumficha mbweha, nyati, chui ama simba lakini hapo ndipo sehemu ambapo watu huja kutambika nyakati tofautitofauti.

Pia maeneo ya kitongoji cha mkuti karibu na kuna kaburi linguine la mmoja wa machifu wa Masasi, Mwenye mkuti, inaonekana kuwa bado anaendelea kukumbukwa na kuheshimiwa kwa kuwa kaburi lake limeifadhiwa katika mazingira mazuri, limesakafiwa na saruji na kufunikwa kwa bati.

Wadau waliwahi kuanzisha Masasi Geographical and Antiquities Association (Maga) kwa madhumuni ya kuweka kumbukumbu za kihistoria kimaandishi, kuanzisha makumbusho na kutembeza watalii. Lakini ndoto haikutimia kwani mzungu aliyehamasisha uanzishwaji wake alipoondoka ikatetereka na kubakia wazo, si tena kitu halisi. Viongozi wapo, niawanayo, lakini kwasababu ya kukosaufadhili Maga haijasonga mbele.

Nadhani kunatatizo katika dhana yautalii. Wengi tuna dhani utalii ni kuona wanyama hasa.  Wengine ni kuona milima. Lakini kuwa utalii ni mjumuisho wa mambo mengi, historia, chakula, mbugazawanyama, uotonakadhalika, ni wazo ambalo halijaenea na hili linapaswa kusisitizwa na wadau kwa sababu ni naamini kuwa kama uhamasishaji na elimu vitaenezwa juu ya maana pana ya utalii na vivutio vya utalii, wageni wataweza kwenda popote Tanzania na hawatakosa kitu cha kujionea.

Kanisa Kuu la Anglika na kwa mfano, lenyewe ni kivutio kikubwa cha utalii. Kuna historia nzuri juu ya kanisa hilo na biashara ya utumwa, elimu na siasa. Pia katik aeneo la mlima mkomaindo kuna msalaba uliwekwa na alama ya V kuandikwa kwenye ukuta wa mwamba wajiwe kuonyesha ushindi wa imani na kuweka ufupisho wa jina la padre wa kwanza wakanisa hilo.

Katika  makaburi hayo niliona mmoja wa mapadri ambaye alikuwa mmoja wa wanafunzi wa kwanza wa Sekondari ya Chidya aliye zaliwa mwaka 1908 na kufa mwaka 2004. Ninani ambaye asingetaka kupata historia ya maisha ya kanisa?

Masasi inatambulishwa kwa misalaba ya kikristo iliyopandwa milimani. Mmoja juu ya Hospitali ya Mkomaindo. Mwingine nyuma ya Sekondari ya Wasichana Masasi kwa ajili yaWakatoliki, na watatu ndiyo huo wa Cathedral lakini hakuna mahali utaweza kupata maelezo kuhusianana kupandishwa mlimani kwa misalaba hiyo. Ni historia inayopotea.

No comments:

Post a Comment