Na Cosmas J. Pahala
Asasi ya kiraia, Ruangwa Decision
Foundation imetoa somo kwa asasi za kiraia wilayani Masasi kwa kuaandaa Siku ya
marafiki Ruangwa, ambayo itaadhimishwa kila mwaka tarehe 20 Februari, ambayo
imeanza kuadhimishwa mwaka huu.
Lengo la kuandaa siku hii ni kutoa
fursa kwa wakazi na wadau wa Ruangwa popote walipo kukutana Ruangwa ili kutoa
msukumo wa kimaendeleo. Maadhimisho hayo yanaenda sambamba na kufanya usafi
maeneo mbalimbali, kutembelea na kutoa misaada kwa wagonjwa, kusaidia watoto
walio katika mazingira magumu na kupanda miti.
Ruangwa Decision Foundation
imeanzishwa hivi karibuni ikiwa na dhamira ya kutoa msukumo wa kimaendeleo
katika maeneo makuu matatu ambayo ni Elimu (elimu ya awali na msingi), Kilimo
na Mazingira. Katika utendaji kazi wake inaongozwa na Kauli Mbiu IBUA HOJA
IJADILIWE.
Wafanyakazi wa asasi mbalimbali za
kiraia Mjini Masasi wakizungumza na Masasi leo, wamesema kuwa hatua iliyofikiwa
na Ruangwa Dicision Foundation imeonesha mwanga na njia kwa asasi za kiraia
zilizopo mjini Masasi na na ukanda wa kusini nzima.
Wilaya ya Ruangwa ni miongoni mwa
wilaya ambazo ziko nyuma kimaendeleo katika nyanja za elimu, kilimo, afya, kiuchumi
na kijamii. Kwa hiyo, Ruangwa Decision Foundation imekuja wakati muafaka na
ujio wake utaleta mapinduzi makubwa kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment